2 Kings 21:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomuua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamtawaza Yosia mwanawe mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamepanga njama dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya fitina juu yake mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomuua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamtawaza Yosia mwanawe mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watu wa nchi wakawaua wote waliopanga hilo shauri baya dhidi ya Mfalme Amoni, nao wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliomfitinia mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomuua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamtawaza Yosia mwanawe mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watu wa nchi hiyo wakawaua wote waliomlia mfalme Amoni njama, kisha hao watu wa nchi hiyo wakamfanya mwanawe Yosia kuwa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya fitina juu yake mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini watu wa Yuda wakawaua wote waliomwua Amoni. Kisha watu hao wa Yuda wakamuweka mwana wake Yosia kuwa mufalme kwa pahali pake.