2 Kings 21:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipoharibiwa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Baali na kutengeneza sanamu ya Ashera, kama vile alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Isitoshe, Manase aliabudu na kutumikia vitu vyote vya mbinguni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia ambapo Hezekia baba yake alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipoharibiwa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Baali na kutengeneza sanamu ya Ashera, kama vile alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Isitoshe, Manase aliabudu na kutumikia vitu vyote vya mbinguni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajenga tena mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo baba yake Hezekia alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akasujudia na kuabudu jeshi lote la angani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akaabudu mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipoharibiwa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Baali na kutengeneza sanamu ya Ashera, kama vile alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Isitoshe, Manase aliabudu na kutumikia vitu vyote vya mbinguni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akavijenga tena vijumba vya kutambikia vilimani, baba yake Hizikia alivyoviangamiza, akaweka nazo meza za kumtambikia Baali, akatengeneza nacho kinyago cha Ashera, kama Ahabu, mfalme wa Waisiraeli, alivyofanya, akaviangukia navyo vikosi vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitengeneza upya nafasi za kuabudia miungu mingine zilizoharibiwa na baba yake Hezekia. Akajenga mazabahu za kuabudia Bali na kutengeneza sanamu ya Ashera, kama vile Ahabu mufalme wa Israeli alivyofanya. Vilevile, Manase aliabudu na kutumikia jeshi la mbingu.