2 Kings 21:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia alimtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa. Alipiga ramli; alibashiri akishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamtoa kafara mwanawe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa Mwenyezi Mungu na kumghadhibisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia alimtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa. Alipiga ramli; alibashiri akishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa BWANA na kumghadhibisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa bwana na kumghadhibisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia alimtoa mwanawe kuwa sadaka ya kuteketezwa. Alipiga ramli; alibashiri akishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata mwanawe akamtumia kuwa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa motoni, tena akaagulia mawingu, akapiga bao, akatumia nao wakweza mizimu na wapunga pepo, akazidi kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, amkasirishe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye alimutoa mwana wake kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Alipiga ramuli; aliaguza akishirikiana na waaguzi wanaosemezana na mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Yawe, akamukasirikisha.