2 Kings 21:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, kiasi kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo Mwenyezi Mungu aliangamiza mbele ya Waisraeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi zaidi kuliko mataifa yale ambayo BWANA aliwaangamiza mbele ya Waisraeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo bwana aliyaangamiza mbele ya Waisraeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa BWANA aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini hawakusikia, naye Manase aliwafanya watende dhambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Mwenyezi-Mungu aliyaharibu mbele ya Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hawakusikia, naye Manase akawaponza kufanya mabaya kuliko wamizimu, Bwana aliowaangamiza mbele ya wana wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa BWANA aliowaharibu mbele za wana wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini hawakusikia, naye Manase aliwasukuma watende zambi zaidi kuliko zile zilizofanywa na mataifa ambayo Yawe aliyaharibu mbele ya Waisraeli.