2 Kings 22:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu wa Yuda wote kuhusu maneno ya kitabu hiki kilichopatikana kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imewaka juu yetu, maana babu zetu hawakutii maneno ya kitabu hiki, na kutimiza yote yaliyoandikwa kutuhusu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nendeni mkamuulize Mwenyezi Mungu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Mwenyezi Mungu ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki. Hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Enendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya Bwana ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu wa Yuda wote kuhusu maneno ya kitabu hiki kilichopatikana kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imewaka juu yetu, maana babu zetu hawakutii maneno ya kitabu hiki, na kutimiza yote yaliyoandikwa kutuhusu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nendeni na mkaulize kwa BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu kile kilichoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya BWANA ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki, hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nendeni mkamuulize bwana kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na Yuda wote kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya bwana ni kubwa inayowaka dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakuyatii maneno ya kitabu hiki. Hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa humo kutuhusu sisi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, kuhusu maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya BWANA ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu wa Yuda wote kuhusu maneno ya kitabu hiki kilichopatikana kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imewaka juu yetu, maana babu zetu hawakutii maneno ya kitabu hiki, na kutimiza yote yaliyoandikwa kutuhusu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nendeni kuniulizia Bwana mimi na ukoo huu na Wayuda wote kwa ajili ya maneno ya hiki kitabu kilichooneka! Kwani makali ya Bwana yenye moto ni makuu, nayo yanatuwakia sisi, kwa kuwa baba zetu hawakuyasikia maneno ya kitabu hiki na kuyafanya yote, tuliyoandikiwa humo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Enendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu hawa, na kwa ajili ya Yuda yote, katika habari za maneno ya kitabu hiki kilichoonekana; kwa kuwa hasira ya BWANA ni kubwa aliyotukasirikia, kwa sababu baba zetu hawakuyaangalia maneno ya kitabu hiki, kufanya kama hayo yote tuliyoandikiwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwende muombe shauri kutoka kwa Yawe kwa ajili yangu, na kwa watu wa Yuda wote juu ya maneno ya kitabu hiki kilichopatikana kwa sababu kasirani ya Yawe imewaka juu yetu, maana babu zetu hawakutii maneno ya kitabu hiki na kutimiza yote yaliyoandikwa juu yetu.”