2 Kings 22:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu wameniacha na kufukizia ubani miungu mingine na hivyo kunikasirisha kwa kazi zote za mikono yao, ghadhabu yangu dhidi ya Yerusalemu itawaka na haitaweza kutulizwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu wameniacha na kufukizia ubani miungu mingine na hivyo kunikasirisha kwa kazi zote za mikono yao, ghadhabu yangu dhidi ya Yerusalemu itawaka na haitaweza kutulizwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa nayo haiwezi kuzimwa.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kunighadhibisha kwa sanamu zote zilizotengenezwa kwa mikono yao, hasira yangu itawaka dhidi ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu wameniacha na kufukizia ubani miungu mingine na hivyo kunikasirisha kwa kazi zote za mikono yao, ghadhabu yangu dhidi ya Yerusalemu itawaka na haitaweza kutulizwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuwa wameniacha, wakavukizia miungu mingine, wanikasirishe kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo makali yangu yenye moto yatapawakia mahali hapa, nayo hayatazimika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu wameniacha mimi, wameifukizia uvumba miungu mingine, ili wapate kunikasirisha kwa kazi yote ya mikono yao; kwa hiyo hasira yangu itawaka juu ya mahali hapa, isizimike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu wameniacha na kufukizia miungu mingine ubani kusudi watu wanikasirikishe kwa kazi zote za mikono yao, basi, kasirani yangu juu ya Yerusalema itawaka na haitaweza kutulizwa.