2 Kings 22:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kiasi cha fedha hizo zipewe wasimamizi wa marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kulipa mishahara ya mafundi wanaofanya marekebisho,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la Mwenyezi Mungu:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya Bwana; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya Bwana, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kiasi cha fedha hizo zipewe wasimamizi wa marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kulipa mishahara ya mafundi wanaofanya marekebisho,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la BWANA:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Waambie waikabidhi kwa watu walioteuliwa kusimamia kazi ya Hekalu. Waamuru watu hawa wawalipe wafanyakazi ambao wanakarabati Hekalu la bwana:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya BWANA, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kiasi cha fedha hizo zipewe wasimamizi wa marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu kulipa mishahara ya mafundi wanaofanya marekebisho,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha wazitie mikononi mwa wenye kazi waliowekwa kuzisimamia kazi za Nyumbani mwa Bwana, nao wawape wazifanyao kazi hizo za Nyumbani mwa Bwana za kupatengeneza, Nyumba ilipobomoka,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena waitie ile fedha katika mikono ya wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA; wakapewe wafanya kazi waliomo ndani ya nyumba ya BWANA, ili wapate kupatengeneza mahali palipobomoka ndani ya nyumba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
nazo zitolewe kwa wale wanaosimamia kazi ya kutengeneza vizuri nyumba ya Yawe kusudi wapate kuwalipa wafundi wanaofanya kazi ya kutengeneza mabomoko,