2 Kings 22:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha kuhani mkuu Hilkia alimwambia katibu Shafani, “Nimekipata Kitabu cha Sheria katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Halafu Hilkia akampatia Shafani kitabu, naye akakisoma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya Bwana. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha kuhani mkuu Hilkia alimwambia katibu Shafani, “Nimekipata Kitabu cha Sheria katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Halafu Hilkia akampatia Shafani kitabu, naye akakisoma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la BWANA.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Torati ndani ya Hekalu la bwana.” Akampa Shafani, ambaye alikisoma.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha Torati katika nyumba ya BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha kuhani mkuu Hilkia alimwambia katibu Shafani, “Nimekipata Kitabu cha Sheria katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.” Halafu Hilkia akampatia Shafani kitabu, naye akakisoma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtambikaji mkuu Hilkia alipomwambia mwandishi Safani: Nimeona kitabu cha Maonyo Nyumbani mwa Bwana. Kisha Hilkia akampa Safani hicho kitabu, akakisoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Kuhani Mukubwa Hilkia akamwambia Safanu, mwandishi: “Nimekipata kitabu cha Sheria katika nyumba ya Yawe.” Halafu Hilkia akamupatia Safanu kitabu, naye akakisoma.