2 Kings 22:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katibu Shafani, alimwendea mfalme na kutoa habari, akisema, “Watumishi wako wametoa fedha zilizopatikana katika nyumba halafu wamezikabidhi kwa mafundi wanaosimamia marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katibu Shafani, alimwendea mfalme na kutoa habari, akisema, “Watumishi wako wametoa fedha zilizopatikana katika nyumba halafu wamezikabidhi kwa mafundi wanaosimamia marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la BWANA na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Shafani mwandishi akamwendea mfalme na kumpa taarifa akisema: “Maafisa wako wametoa ile fedha ambayo ilikuwa ndani ya Hekalu la bwana na imekabidhiwa mikononi mwa wasimamizi wa marekebisho ya Hekalu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katibu Shafani, alimwendea mfalme na kutoa habari, akisema, “Watumishi wako wametoa fedha zilizopatikana katika nyumba halafu wamezikabidhi kwa mafundi wanaosimamia marekebisho ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwandishi Safani akaja kwa mfalme, akampasha mfalme habari na kumwambia: watumishi wako wamezimimina fedha zilizoonekana Nyumbani mwa Bwana, wakazitia mikononi mwao wenye kazi waliowekwa kuisimamia Nyumba ya Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Shafani mwandishi akamwendea mfalme, akamletea mfalme habari tena, akasema, Watumishi wako wamezitoa zile fedha zilizoonekana ndani ya nyumba, nao wamewakabidhi wafanya kazi wanaoisimamia nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwandishi Safanu akamwendea mufalme na kutoa habari, akisema: “Watumishi wako wametoa feza zilizopatikana katika nyumba, halafu wakazipeleka kwa wafundi wanaosimamia kazi ya kutengeneza nyumba ya Yawe.”