2 Kings 23:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kadhalika aliondoa farasi waliotengwa na wafalme wa Yuda kwa ajili ya jua, kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, karibu na chumba cha Nathan-meleki, kilichokuwa kiungani; naye alichoma kwa moto magari ya jua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaondoa kutoka ingilio la Hekalu la Mwenyezi Mungu wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathan-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari ya vita yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa jua.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa Bwana, karibu na chumba cha Nathan-Meleki, towashi, kilichohuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kadhalika aliondoa farasi waliotengwa na wafalme wa Yuda kwa ajili ya jua, kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, karibu na chumba cha Nathan-meleki, kilichokuwa kiungani; naye alichoma kwa moto magari ya jua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaondoa kutoka kwenye ingilio la Hekalu la BWANA wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya mungu jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathani-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa mungu jua.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaondoa kutoka kwenye ingilio la Hekalu la bwana wale farasi ambao wafalme wa Yuda walikuwa wamewaweka wakfu kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye ua karibu na chumba cha afisa aliyeitwa Nathan-Meleki. Basi Yosia akayachoma moto yale magari yaliyokuwa yamewekwa wakfu kwa jua.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa BWANA, karibu na chumba cha Nathan-Meleki, towashi, kilichokuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kadhalika aliondoa farasi waliotengwa na wafalme wa Yuda kwa ajili ya jua, kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, karibu na chumba cha Nathan-meleki, kilichokuwa kiungani; naye alichoma kwa moto magari ya jua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawakomesha nao wale farasi, wafalme wa Wayuda waliowekea jua hapo pa kuingia Nyumbani mwa Bwana karibu ya chumba cha kulalia cha mtumishi wa nyumbani Natani-Meleki kilichokuwa katika kijumba kile kilichojengwa upande wa machweoni kwa jua, nayo magari ya jua akayateketeza motoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaondoa farasi ambao wafalme wa Yuda waliwatoa kwa jua, hapo pa kuingia nyumbani mwa BWANA, karibu na chumba cha Nathan-Meleki, towashi, kilichohuwako kiungani; akayapiga moto magari ya jua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile aliondoa farasi waliotengwa na wafalme wa Yuda kwa ajili ya kuabudu jua kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Yawe, karibu na chumba cha Natani-Meleki, kilichokuwa inje ya muji; naye alichoma kwa moto magari ya jua.