2 Kings 23:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Madhabahu ambayo wafalme wa Yuda walijenga paani kwenye chumba cha juu cha Ahazi, pamoja na madhabahu ambayo Manase alijenga katika nyua mbili za nyumba ya Mwenyezi-Mungu aliyabomoa na kuyapondaponda, kisha alitupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la Mwenyezi Mungu. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande, na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya Bwana, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Madhabahu ambayo wafalme wa Yuda walijenga paani kwenye chumba cha juu cha Ahazi, pamoja na madhabahu ambayo Manase alijenga katika nyua mbili za nyumba ya Mwenyezi-Mungu aliyabomoa na kuyapondaponda, kisha alitupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la BWANA. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alizivunja madhabahu ambazo wafalme wa Yuda walikuwa wamezijenga kwenye paa la ghorofa ya Ahazi, pia madhabahu alizokuwa amezijenga Manase katika nyua mbili za Hekalu la bwana. Akaziondoa huko, akazivunja vipande vipande, na kutupa hicho kifusi katika Bonde la Kidroni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya BWANA, mfalme akazivunja, akaziteremsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Madhabahu ambayo wafalme wa Yuda walijenga paani kwenye chumba cha juu cha Ahazi, pamoja na madhabahu ambayo Manase alijenga katika nyua mbili za nyumba ya Mwenyezi-Mungu aliyabomoa na kuyapondaponda, kisha alitupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo meza za kutambikia zilizokuwa darini penye chumba cha juu cha Ahazi zilizotengenezwa na wafalme wa Wayuda nazo meza za kutambikia, Manase alizozitengeneza katika nyua zote mbili za Nyumba ya Bwana, mfalme akazivunjavunja na kuzitoa hapo, kisha akayatupa mavumbi yao katika mto wa Kidoroni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nazo madhabahu zilizokuwako darini juu ya chumba cha juu cha Ahazi, wafalme wa Yuda walizozifanya, nazo madhabahu alizozifanya Manase katika behewa mbili za nyumba ya BWANA, mfalme akazivunja, akazitelemsha huko nje, na kuyatupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazabahu ambayo wafalme wa Yuda walijenga juu ya paa kwenye chumba cha juu cha Ahazi, pamoja na mazabahu ambayo Manase alijenga katika viwanja viwili vya nyumba ya Yawe, aliyabomoa na kuyapondaponda, kisha alitupa mavumbi yake katika kijito cha Kidroni.