2 Kings 23:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme pia alipatia unajisi mahali pa kuabudia palipokuwa upande wa mashariki ya Yerusalemu na kuelekea upande wa mlima wa Ufisadi, mahali mfalme wa Israeli alipopajenga kwa ajili ya Ashtarothi chukizo la Wasidoni, Kemoshi chukizo la Moabu na pia kwa ajili ya Milkomu chukizo la Waamoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme pia akanajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, zilizokuwa mashariki mwa Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amejenga mahali pa kuabudia kwa ajili ya Ashtorethi mungu wa kike wa Wasidoni, aliyekuwa chukizo; na kwa ajili ya Kemoshi mungu wa Wamoabu, aliyekuwa chukizo; na kwa ajili ya Moleki mungu wa watu wa Amoni, aliyekuwa chukizo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme pia alipatia unajisi mahali pa kuabudia palipokuwa upande wa mashariki ya Yerusalemu na kuelekea upande wa mlima wa Ufisadi, mahali mfalme wa Israeli alipopajenga kwa ajili ya Ashtarothi chukizo la Wasidoni, Kemoshi chukizo la Moabu na pia kwa ajili ya Milkomu chukizo la Waamoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme pia akapaharibu mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke aliye chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi yule mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu aliye chukizo la watu wa Amoni, pasifae tena kufanyia hizo ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme pia akanajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, palipokuwa mashariki ya Yerusalemu upande wa kusini wa Kilima cha Uharibifu, pale ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amejenga kwa ajili ya Ashtorethi mungu mke chukizo la Wasidoni, kwa ajili ya Kemoshi mungu chukizo la Wamoabu, na kwa ajili ya Moleki mungu chukizo la watu wa Amoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kulia wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme pia alipatia unajisi mahali pa kuabudia palipokuwa upande wa mashariki ya Yerusalemu na kuelekea upande wa mlima wa Ufisadi, mahali mfalme wa Israeli alipopajenga kwa ajili ya Ashtarothi chukizo la Wasidoni, Kemoshi chukizo la Moabu na pia kwa ajili ya Milkomu chukizo la Waamoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme akavichafua navyo vijumba vya vilimani pa kutambikia vilivyoko ng'ambo ya Yerusalemu kuumeni kwenye Mlima wa Mwangamizaji, Salomo, mfalme wa Waisiraeli, alivyovijenga vya kutambikia Astoreti, lile tapisho la Wasidoni, na Kemosi, lile tapisho la Wamoabu, na Milkomu, lile chukizo la wana wa amoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kuume wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile aliharibu pahali pa kuabudia palipokuwa upande wa mashariki ya Yerusalema na kuelekea upande wa mulima wa uharibifu, pahali mufalme wa Israeli alipopajenga kwa ajili ya Astaroti chukizo la Wasidoni, Kemosi chukizo la Moabu na vilevile kwa ajili ya Milkomu chukizo la Waamoni.