2 Kings 23:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Zaidi ya hayo aliharibu huko Betheli mahali pa kuabudia palipojengwa na mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewafanya watu wa Israeli watende dhambi; aliharibu madhabahu hayo na kuvunja mawe yake katika vipandevipande, na kisha akaviponda mpaka vikawa vumbi; pia akachoma sanamu ya Ashera.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata madhabahu yaliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, alibomoa hata hayo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia na kupasaga hadi pakawa vumbi, na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli, madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali pa juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile Ashera.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Zaidi ya hayo aliharibu huko Betheli mahali pa kuabudia palipojengwa na mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewafanya watu wa Israeli watende dhambi; aliharibu madhabahu hayo na kuvunja mawe yake katika vipandevipande, na kisha akaviponda mpaka vikawa vumbi; pia akachoma sanamu ya Ashera.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata madhabahu iliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, hata hiyo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia miungu alipabomoa. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia miungu na kupasaga hadi pakawa vumbi na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata madhabahu yaliyokuwa huko Betheli, mahali pa juu pa kuabudia miungu palipokuwa pamejengwa na Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye aliwafanya Israeli watende dhambi, alibomoa hata hayo madhabahu na mahali pa juu pa kuabudia miungu. Alipateketeza kwa moto hapo mahali pa juu pa kuabudia miungu na kupasaga hadi pakawa vumbi, na kuichoma hiyo nguzo ya Ashera pia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli, madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali pa juu alipateketeza, akapapondaponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile Ashera.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Zaidi ya hayo aliharibu huko Betheli mahali pa kuabudia palipojengwa na mfalme Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewafanya watu wa Israeli watende dhambi; aliharibu madhabahu hayo na kuvunja mawe yake katika vipandevipande, na kisha akaviponda mpaka vikawa vumbi; pia akachoma sanamu ya Ashera.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaivunjavunja nayo meza ya kutambikia iliyokuwa Beteli kilimani. Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Waisiraeli, alikotengeneza kijumba cha kutambikia; basi, ile meza yenyewe pamoja na kijumba cha kutambikia pale kilimani akaivunjavunja, kisha yote pia yaliyokuwako huko kilimani akayateketeza kwa moto, akayapondaponda, yawe mavumbi tu, hata kinyago cha Ashera akakiteketeza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena zaidi ya hayo, ile madhabahu iliyokuwako Betheli, na mahali pa juu alipopafanya Yeroboamu, mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli, madhabahu hiyo aliibomoa; na mahali pa juu alipateketeza, akapaponda-ponda hata pakawa mavumbi, akaiteketeza ile Ashera.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Zaidi ya hayo aliharibu kule Beteli pahali pa kuabudia palipojengwa na mufalme Yeroboamu mwana wa Nebati ambaye aliwasukuma watu wa Israeli watende zambi. Aliharibu mazabahu hayo na kuvunja mawe yake vipandevipande, na kisha akaviponda mpaka vikakuwa mavumbi. Vilevile akachoma sanamu ya Ashera.