2 Kings 23:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yosia alipogeuka aliona makaburi juu ya kilima; aliagiza mifupa ifukuliwe kutoka makaburini na kuichoma juu ya madhabahu; basi akayatia unajisi madhabahu sawasawa na neno la Mwenyezi-Mungu ambalo mtu wa Mungu alilitangaza, nabii ambaye alitabiri matukio haya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitendeka kulingana na neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la Bwana, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yosia alipogeuka aliona makaburi juu ya kilima; aliagiza mifupa ifukuliwe kutoka makaburini na kuichoma juu ya madhabahu; basi akayatia unajisi madhabahu sawasawa na neno la Mwenyezi-Mungu ambalo mtu wa Mungu alilitangaza, nabii ambaye alitabiri matukio haya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Yosia akatazamatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu hiyo ya Betheli ili kupafanya pasifae tena kufanyia hizo ibada za miungu. Hili lilitokea sawasawa na neno la BWANA lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Yosia akatazama huku na huko, naye alipoona makaburi yaliyokuwa huko kwenye kilima, akaamuru mifupa itolewe humo na akaichoma juu ya madhabahu ya Betheli ili kupanajisi. Hili lilitokea kulingana na neno la bwana lililosemwa na mtu wa Mungu ambaye alitangulia kusema mambo haya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la BWANA, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yosia alipogeuka aliona makaburi juu ya kilima; aliagiza mifupa ifukuliwe kutoka makaburini na kuichoma juu ya madhabahu; basi akayatia unajisi madhabahu sawasawa na neno la Mwenyezi-Mungu ambalo mtu wa Mungu alilitangaza, nabii ambaye alitabiri matukio haya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yosia alipogeuka akaona makaburi yaliyokuwa katika mlima ule, akatuma kuichukua mifupa iliyokuwa mle makaburini, akaiteketeza juu ya meza ya kutambikia, akaichafua hivyo kwa lile neno la Bwana, alilolitangaza yule mtu wa Mungu aliyeyatangaza mambo haya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yosia alipogeuka, aliyaona makaburi yale yaliyokuwako huko, juu ya mlima; akatuma watu, akaitoa ile mifupa katika yale makaburi, akaiteketeza juu ya madhabahu, akainajisi, sawasawa na lile neno la BWANA, alilolinena yule mtu wa Mungu, aliyetamka mambo hayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yosia alipogeuka akaona makaburi juu ya kilima. Aliagiza mifupa ifukuliwe kutoka makaburi na kuichoma juu ya mazabahu. Basi akachafua mazabahu sawasawa na neno la Yawe ambalo mutu wa Mungu alilitangaza, nabii ambaye alitabiri matukio haya.