2 Kings 23:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye mfalme akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akifuatana na watu wote wa Yuda na wakazi wote wa Yerusalemu, na makuhani pamoja na manabii, watu wote wadogo kwa wakubwa. Basi, akawasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akapanda kwenda hekaluni mwa Mwenyezi Mungu pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, kilichokuwa kimepatikana katika Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa Bwana, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye mfalme akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akifuatana na watu wote wa Yuda na wakazi wote wa Yerusalemu, na makuhani pamoja na manabii, watu wote wadogo kwa wakubwa. Basi, akawasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akapanda mpaka kwenye Hekalu la BWANA pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote kuanzia aliye mdogo hadi aliye mkubwa kabisa. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akapanda kwenda hekaluni mwa bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na manabii, watu wote wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa BWANA, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya Kitabu cha Agano kilichoonekana katika nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye mfalme akaenda katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu akifuatana na watu wote wa Yuda na wakazi wote wa Yerusalemu, na makuhani pamoja na manabii, watu wote wadogo kwa wakubwa. Basi, akawasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme akapanda kwenda Nyumbani mwa Bwana pamoja na Wayuda wote na wenyeji wote wa Yerusalemu na watambikaji na wafumbuaji na watu wote pia, wadogo kwa wakubwa, wakaenda naye, akawasomea masikioni pao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichooneka Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mfalme akapanda kwenda nyumbani kwa BWANA, na watu wote wa Yuda, nao wote waliokaa Yerusalemu, pamoja naye, na makuhani, na manabii, na watu wote, wadogo kwa wakubwa; akasoma masikioni mwao maneno yote ya kitabu cha agano kilichoonekana katika nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye mufalme akaenda katika nyumba ya Yawe pamoja na watu wote wa Yuda na wakaaji wote wa Yerusalema, na makuhani pamoja na manabii, watu wote, wadogo kwa wakubwa. Basi, akawasomea maneno ya kitabu cha agano kilichopatikana katika nyumba ya Yawe.