2 Kings 23:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliwaua makuhani wote wa miungu ya uongo juu ya madhabahu ambapo walitumikia na kuchoma mifupa yao juu ya madhabahu hayo. Kisha alirudi Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia katika madhabahu zao wenyewe, na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliwaua makuhani wote wa miungu ya uongo juu ya madhabahu ambapo walitumikia na kuchoma mifupa yao juu ya madhabahu hayo. Kisha alirudi Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika madhabahu zao wenyewe na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yosia akawachinja makuhani wote wa mahali pa juu pa kuabudia miungu katika madhabahu zao wenyewe, na kuchoma mifupa ya wanadamu juu yake. Kisha akarudi Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliwaua makuhani wote wa miungu ya uongo juu ya madhabahu ambapo walitumikia na kuchoma mifupa yao juu ya madhabahu hayo. Kisha alirudi Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watambikaji wote wa vilimani waliokuwako huko akawachinja, wawe ng'ombe za tambiko juu ya zile meza za kutambikia, hata mifupa ya watu akaiteketeza juu yao, kisha akarudi Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaua na makuhani wote wa mahali pa juu waliokuwako huko, juu ya madhabahu, akateketeza mifupa ya watu juu yake; kisha akarejea Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Aliwaua makuhani wote wa miungu ya uongo juu ya mazabahu ambapo walitumikia na kuchoma mifupa yao juu ya mazabahu hayo. Kisha akarudi Yerusalema.