2 Kings 23:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, ili mfalme Yosia atekeleze sheria zote zilizoandikwa katika kitabu alichokipata kuhani mkuu Hilkia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliondoa katika nchi ya Yuda na Yerusalemu, wachawi, watabiri, vinyago vya miungu, sanamu za miungu pamoja na vitu vyote vya kuchukiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa waaguzi, waabudu mizimu, miungu ya nyumbani, sanamu za kuabudiwa, na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana huko Yuda na Yerusalemu. Aliyafanya haya ili kutimiza matakwa ya sheria iliyoandikwa katika kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikipata ndani ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, ili mfalme Yosia atekeleze sheria zote zilizoandikwa katika kitabu alichokipata kuhani mkuu Hilkia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliondoa katika nchi ya Yuda na Yerusalemu, wachawi, watabiri, vinyago vya miungu, sanamu za miungu pamoja na vitu vyote vya kuchukiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa wapunga pepo, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana katika Yuda na Yerusalemu. Haya aliyafanya ili kutimiza itakiwavyo kulingana na sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikikuta ndani ya Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo, Yosia akawaondoa waaguzi, wanaoabudu mizimu, sanamu za kuagulia, sanamu za kuabudiwa, na vitu vingine vyote vya machukizo vilivyoonekana huko Yuda na Yerusalemu. Aliyafanya haya ili kutimiza matakwa ya sheria iliyoandikwa ndani ya kile kitabu ambacho Hilkia kuhani alikipata ndani ya Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, ili mfalme Yosia atekeleze sheria zote zilizoandikwa katika kitabu alichokipata kuhani mkuu Hilkia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, aliondoa katika nchi ya Yuda na Yerusalemu, wachawi, watabiri, vinyago vya miungu, sanamu za miungu pamoja na vitu vyote vya kuchukiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakweza mizimu na wapunga pepo na vinyago vya nyumbani na magogo ya kutambikia na matapisho yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda namo Yerusalemu Yosia akayaondoa, kusudi ayatimize maneno ya Maonyo yaliyoandikwa katika kile kitabu, mtambikaji Hilkia alichokiona Nyumbani mwa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena wenye pepo wa utambuzi, na wachawi, na vinyago, na sanamu, na machukizo yote yaliyoonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, Yosia akayaondoa yote, ili apate kuyathibitisha maneno ya torati yaliyoandikwa katika kile kitabu alichokiona Hilkia kuhani ndani ya nyumba ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, kusudi mufalme Yosia atimize sheria zote zilizoandikwa katika kitabu Kuhani Mukubwa Hilkia alichokipata katika nyumba ya Yawe, aliondoa wachawi, watabiri, miungu, sanamu za miungu pamoja na vyombo vingine vilivyotumika kwa kuabudu miungu ya uongo kutoka inchi ya Yuda na kutoka Yerusalema.