2 Kings 23:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kabla ya Yosia au baada yake hakuna mfalme yeyote aliyekuwa kama yeye, ambaye alimtumikia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote, kwa nguvu zake zote na kwa roho yake yote kulingana na sheria ya Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hapakuwepo mfalme mwingine kabla na baada ya Yosia aliyempenda Mwenyezi Mungu kama yeye; kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, kulingana na Torati yote ya Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kabla ya Yosia au baada yake hakuna mfalme yeyote aliyekuwa kama yeye, ambaye alimtumikia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote, kwa nguvu zake zote na kwa roho yake yote kulingana na sheria ya Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kabla wala baada ya Mfalme Yosia hapakuwepo na mfalme mwingine ye yote ambaye alimpenda BWANA kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria yote ya Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kabla wala baada ya Yosia, hapakuwepo na mfalme mwingine yeyote ambaye alimpenda bwana kwa moyo wake wote, kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Torati yote ya Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria ya Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kabla ya Yosia au baada yake hakuna mfalme yeyote aliyekuwa kama yeye, ambaye alimtumikia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wake wote, kwa nguvu zake zote na kwa roho yake yote kulingana na sheria ya Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfalme kama yeye hakuwako mbele yake aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote na kwa nguvu yake yote, ayafanye Maonyo yote ya Mose, wala nyuma yake hakuondokea aliyekuwa kama yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mbele ya Yosia au nyuma yake hakuna mufalme yeyote aliyekuwa kama yeye, ambaye alimutumikia Yawe kwa moyo wake wote, kwa nguvu zake zote na kwa roho yake yote kulingana na Sheria ya Musa.