2 Kings 23:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu alisema, “Nitawafukuza watu wa Yuda kutoka mbele yangu kama vile nilivyofanya kwa watu wa Israeli; nitaukataa mji wa Yerusalemu ambao niliuchagua niliposema, ‘Jina langu litakuwa humo.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Mwenyezi Mungu akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua, na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Jina langu litakaa humo.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu alisema, “Nitawafukuza watu wa Yuda kutoka mbele yangu kama vile nilivyofanya kwa watu wa Israeli; nitaukataa mji wa Yerusalemu ambao niliuchagua niliposema, ‘Jina langu litakuwa humo.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo BWANA akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Humo Jina langu litakaa.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo bwana akasema, “Nitamwondoa Yuda mbele zangu kama nilivyomwondoa Israeli, nami nitaukataa Yerusalemu, mji niliouchagua, na Hekalu hili, ambalo nilisema, ‘Jina langu litakaa humo.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu alisema, “Nitawafukuza watu wa Yuda kutoka mbele yangu kama vile nilivyofanya kwa watu wa Israeli; nitaukataa mji wa Yerusalemu ambao niliuchagua niliposema, ‘Jina langu litakuwa humo.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana akasema: Wayuda nao nitawaondoa usoni pangu, kama nilivyowaondoa Waisiraeli, tena nitautupa nao mji huu wa Yerusalemu, niliouchagua, nayo Nyumba hii, niliyoisema: Jina langu litakaa humu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe akasema: “Nitawafukuza watu wa Yuda kutoka mbele yangu kama vile nilivyofanya kwa watu wa Israeli. Nitaukataa muji wa Yerusalema ambao niliuchagua niliposema: ‘Jina langu litakuwa mule.’ ”