2 Kings 23:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maofisa wake wakaibeba maiti yake katika gari na kuirejesha Yerusalemu walikomzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa Yuda wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia wakampaka mafuta na kumtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakampaka mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watumishi wake wakamchukua garini, amekwisha kufa, kutoka Megido, wakamleta Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake mwenyewe. Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, wakamtawaza awe mfalme badala ya baba yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maofisa wake wakaibeba maiti yake katika gari na kuirejesha Yerusalemu walikomzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa Yuda wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia wakampaka mafuta na kumtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake ndani ya gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watumishi wa Yosia wakauleta mwili wake katika gari la vita kutoka Megido hadi Yerusalemu, wakamzika kwenye kaburi lake mwenyewe. Nao watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta na kumfanya mfalme mahali pa baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watumishi wake wakamchukua garini, amekwisha kufa, kutoka Megido, wakamleta Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake mwenyewe. Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, wakamtawaza awe mfalme badala ya baba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maofisa wake wakaibeba maiti yake katika gari na kuirejesha Yerusalemu walikomzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa Yuda wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia wakampaka mafuta na kumtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watumishi wake wakamchukua garini, alipokwisha kufa, wakamtoa Megido na kumpeleka Yerusalemu, wakamzika kaburini mwake. Kisha watu wa nchi hii wakamchukua Yoahazi, mwana wa Yosia, wakampaka mafuta, wakamfanya kuwa mfalme mahali pa baba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watumishi wake wakamchukua garini, amekwisha kufa, kutoka Megido, wakamleta Yerusalemu, wakamzika katika kaburi lake mwenyewe. Watu wa nchi wakamtwaa Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, wakamtawaza awe mfalme badala ya baba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wake wakaibeba maiti yake katika gari na kuirudisha Yerusalema walikomuzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa Yuda wakamuchukua Yoahazi mwana wa Yosia, wakamupakaa mafuta na kumuweka kuwa mufalme kwa pahali pa baba yake.