2 Kings 23:33 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ili asiendelee kutawala huko Yerusalemu, Farao Neko alimtia nguvuni huko Ribla katika nchi ya Hamathi, akaitoza nchi kodi ya kilo 3,400 za madini ya fedha na kilo 34 za dhahabu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja za fedha, na talanta moja ya dhahabu katika Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Farao-neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia za fedha na talanta ya dhahabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ili asiendelee kutawala huko Yerusalemu, Farao Neko alimtia nguvuni huko Ribla katika nchi ya Hamathi, akaitoza nchi kodi ya kilo 3,400 za madini ya fedha na kilo 34 za dhahabu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Farao Neko akamfunga katika minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili kwamba asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akaamuru kodi ya talanta 100 za fedha na talanta ya dhahabu katika Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Farao Neko akamfunga kwa minyororo huko Ribla katika nchi ya Hamathi ili asiweze kutawala huko Yerusalemu, naye akatoza kodi ya talanta mia moja za fedha, na talanta moja ya dhahabu katika Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Farao Neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia moja za fedha na talanta ya dhahabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ili asiendelee kutawala huko Yerusalemu, Farao Neko alimtia nguvuni huko Ribla katika nchi ya Hamathi, akaitoza nchi kodi ya kilo 3,400 za madini ya fedha na kilo 34 za dhahabu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Farao Neko akamfunga huko Ribula katika nchi ya Hamati, asiwe mfalme mle Yerusalemu, akailipisha nchi hii vipande 100 vya fedha, ndio shilingi milioni na 200000, na kipande kimoja cha dhahabu, ndio shilingi 220000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Farao-neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia za fedha na talanta ya dhahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kusudi asiendelee kutawala akiwa kule Yerusalema, Neko mufalme wa Misri alimufunga kule Ribla katika inchi ya Hamati, akawalipisha watu wa Yuda kodi ya kilo elfu tatu na mia ine za feza na kilo makumi tatu na ine za zahabu.