2 Kings 23:35 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Yehoyakimu alimpa Farao fedha na dhahabu, lakini aliitoza nchi kodi ili aweze kutekeleza matakwa ya Farao ya kupewa fedha. Aliwatoza wananchi fedha na dhahabu. Kila mmoja alitoa kiasi alichokadiria mfalme, naye akampa Farao Neko.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoyakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadirio ya mapato yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao-neko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Yehoyakimu alimpa Farao fedha na dhahabu, lakini aliitoza nchi kodi ili aweze kutekeleza matakwa ya Farao ya kupewa fedha. Aliwatoza wananchi fedha na dhahabu. Kila mmoja alitoa kiasi alichokadiria mfalme, naye akampa Farao Neko.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoiakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoiakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadrio ya mapato yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoyakimu akamlipa Farao Neko ile fedha na dhahabu aliyodai. Ili kuweza kufanya hivyo, Yehoyakimu akatoza nchi kodi na kulipiza fedha na dhahabu kutoka kwa watu wa nchi kulingana na makadrio ya mapato yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao Neko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Yehoyakimu alimpa Farao fedha na dhahabu, lakini aliitoza nchi kodi ili aweze kutekeleza matakwa ya Farao ya kupewa fedha. Aliwatoza wananchi fedha na dhahabu. Kila mmoja alitoa kiasi alichokadiria mfalme, naye akampa Farao Neko.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zile fedha na dhahabu Yoyakimu akampa Farao; lakini hakuwa na budi kuitoza nchi machango, apate kuzilipa hizo fedha, Farao alizozitaka; watu wa hiyo nchi yake akamtoza kila mmoja kwa mali, alizowaziwa kuwa nazo; ndivyo, alivyowachangisha hizo fedha na dhahabu za kumpa Farao Neko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yehoyakimu akampa Farao dhahabu na fedha; lakini akaitoza nchi kodi, ili apate kutoa zile fedha kwa amri yake Farao; akawatoza fedha na dhahabu watu wa nchi, kila mtu kwa kodi yake, ili ampe Farao-neko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Yoyakimu akamupa Mufalme wa Misri feza na zahabu, lakini akailipisha inchi kodi kusudi aweze kutimiza mapenzi ya Mufalme wa Misri ya kupewa feza. Akawalipisha wanainchi feza na zahabu. Kila mumoja alitoa kufuatana na kiasi mufalme alichoamuru, naye akamupa Neko mufalme wa Misri.