2 Kings 23:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Aliondoa Ashera kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya Yerusalemu, akaipeleka mpaka kijito cha Kidroni. Huko akaiteketeza na kuisaga mpaka ikawa mavumbi, nayo mavumbi yake akayatawanya juu ya makaburi ya watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu, na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu, akaiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wasio na cheo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya Bwana, nje ya Yerusalemu, mpaka Kidroni, akaipiga moto penye kijito cha Kidroni, na kuiponda-ponda iwe mavumbi, akayatupa mavumbi yake juu ya makaburi ya watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Aliondoa Ashera kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya Yerusalemu, akaipeleka mpaka kijito cha Kidroni. Huko akaiteketeza na kuisaga mpaka ikawa mavumbi, nayo mavumbi yake akayatawanya juu ya makaburi ya watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu la BWANA na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu na kuiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wabaya ambao waliitolea kafara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaiondoa nguzo ya Ashera kutoka kwenye Hekalu la bwana, na kuipeleka kwenye Bonde la Kidroni nje ya Yerusalemu, akaiteketeza huko. Akaisaga hadi ikawa unga na kusambaza hilo vumbi juu ya makaburi ya watu wa kawaida.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya BWANA, nje ya Yerusalemu, mpaka Kidroni, akaipiga moto penye kijito cha Kidroni, na kuipondaponda iwe mavumbi, akayatupa mavumbi yake juu ya makaburi ya watu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Aliondoa Ashera kutoka katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, nje ya Yerusalemu, akaipeleka mpaka kijito cha Kidroni. Huko akaiteketeza na kuisaga mpaka ikawa mavumbi, nayo mavumbi yake akayatawanya juu ya makaburi ya watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho kinyago kile cha Ashera akakitoa Nyumbani mwa Bwana na kukipeleka nje ya Yerusalemu kwenye mto wa Kidoroni, akakichoma moto huko kwenye mto wa Kidoroni na kukipondaponda, kiwe mavumbi tu, nayo hayo mavumbi akayatupa kwenye makaburi yao walio watuwatu tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye akaiondoa Ashera katika nyumba ya BWANA, nje ya Yerusalemu, mpaka Kidroni, akaipiga moto penye kijito cha Kidroni, na kuiponda-ponda iwe mavumbi, akayatupa mavumbi yake juu ya makaburi ya watu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye aliondoa sanamu ya Ashera kutoka katika nyumba ya Yawe, inje ya Yerusalema, akaipeleka mpaka kwenye kijito cha Kidroni. Kule akaiteketeza na kuisaga mpaka ikakuwa mavumbi, nayo mavumbi yake akayatawanya juu ya makaburi ya watu.