2 Kings 23:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akakusanya makuhani wote kutoka miji ya Yuda na akapatia najisi mahali pa juu makuhani walikofukiza ubani, kutoka Geba mpaka Beer-sheba; naye akabomoa mahali pa juu palipokuwa upande wa kushoto wa lango la mji penye malango yaliyokuwa kwenye njia ya kuingilia lango la Yoshua mtawala wa mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yosia akawaleta makuhani wote wa Mwenyezi Mungu kutoka miji yote ya Yuda, na kunajisi mahali pa juu pa kuabudia, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la Lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu, makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, liwali wa mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akakusanya makuhani wote kutoka miji ya Yuda na akapatia najisi mahali pa juu makuhani walikofukiza ubani, kutoka Geba mpaka Beer-sheba; naye akabomoa mahali pa juu palipokuwa upande wa kushoto wa lango la mji penye malango yaliyokuwa kwenye njia ya kuingilia lango la Yoshua mtawala wa mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosia akawaleta makuhani wote wa BWANA kutoka miji yote ya Yuda na kupafanya mahali pa juu pa kuabudia miungu pasifae tena kufanyia hizo ibada, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yosia akawaleta makuhani wote wa bwana kutoka miji yote ya Yuda, na kunajisi mahali pa juu pa kuabudia miungu, kuanzia Geba hadi Beer-Sheba, mahali pote ambapo hao makuhani wa miungu walifukiza uvumba. Akabomoa mahali pa kuwekea vitu vya ibada za miungu palipokuwa katika malango, kwenye ingilio la Lango la Yoshua, mtawala wa mji, lililoko upande wa kushoto wa lango la mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu, makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, mtawala wa mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akakusanya makuhani wote kutoka miji ya Yuda na akapatia najisi mahali pa juu makuhani walikofukiza ubani, kutoka Geba mpaka Beer-sheba; naye akabomoa mahali pa juu palipokuwa upande wa kushoto wa lango la mji penye malango yaliyokuwa kwenye njia ya kuingilia lango la Yoshua mtawala wa mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watambikaji wote akawatoa katika miji ya Wayuda, akavichafua vijumba vya vilimani, hao watambikaji walimovukizia toka Geba mpaka Beri-Seba, navyo vijumba vya kutambikia vilimani vilivyokuwa malangoni upande wa kushoto wa hapo pa kuliingilia lango la Yosua, mkuu wa mji, watu walipoingia mjini, navyo akavibomoa kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawatoa makuhani wote katika miji ya Yuda, akapanajisi mahali pa juu, makuhani walipokuwa wamefukiza uvumba, tangu Geba hata Beer-sheba; akapavunja mahali pa juu pa malango, palipokuwapo penye kuingia lango la Yoshua, liwali wa mji, palipokuwa upande wa kushoto wa mtu langoni pa mji.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akakusanya makuhani wote kutoka miji ya Yuda na aliharibu pahali pa kuabudia makuhani walipofukiza ubani, kutoka Geba mpaka Beri-Seba. Akabomoa pahali pa kuabudia palipokuwa upande wa kushoto wa mulango wa muji kwenye milango iliyokuwa kwenye njia ya kuingilia kwenye mulango wa Yoshua mutawala wa muji.