2 Kings 23:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makuhani hao hawakufikia madhabahu ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu, lakini walikula mikate isiyotiwa chachu waliyopewa na jamaa zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia hawakuhudumu katika madhabahu ya Mwenyezi Mungu katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu pamoja na ndugu zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini hao makuhani wa mahali pa juu hawakupanda madhabahuni kwa Bwana katika Yerusalemu, bali wakala mikate isiyo na chachu katikati ya ndugu zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makuhani hao hawakufikia madhabahu ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu, lakini walikula mikate isiyotiwa chachu waliyopewa na jamaa zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu hawakuhudumu katika madhabahu ya BWANA katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa makuhani wa mahali pa juu pa kuabudia miungu hawakuhudumu katika madhabahu ya bwana katika Yerusalemu, walikula mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini hao makuhani wa mahali pa juu hawakupanda madhabahuni kwa BWANA katika Yerusalemu, bali wakala mikate isiyo na chachu katikati ya ndugu zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makuhani hao hawakufikia madhabahu ya Mwenyezi-Mungu katika Yerusalemu, lakini walikula mikate isiyotiwa chachu waliyopewa na jamaa zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wale watambikaji wa vilimani hawakupata ruhusa kutambika penye meza ya kumtambikia Bwana mle Yerusalemu, wakala tu kwa ndugu zao mikate isiyochachwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini hao makuhani wa mahali pa juu hawakupanda madhabahuni kwa BWANA katika Yerusalemu, bali wakala mikate isiyo na chachu katikati ya ndugu zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makuhani hao hawakufikia mazabahu ya Yawe katika Yerusalema, lakini walikula mikate isiyotiwa chachu waliyopewa na makuhani wenzao.