2 Kings 24:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na Yehoyakini mfalme wa Yuda alijisalimisha kwa mfalme wa Babuloni, yeye mwenyewe pamoja na mama yake, watumishi wake, maofisa na maakida wake. Mfalme wa Babuloni alimchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na Yehoyakini mfalme wa Yuda alijisalimisha kwa mfalme wa Babuloni, yeye mwenyewe pamoja na mama yake, watumishi wake, maofisa na maakida wake. Mfalme wa Babuloni alimchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoyakini mfalme wa Yuda, mama yake, wahudumu wake, wakuu na maafisa wake wote wakajisalimisha kwa Nebukadneza. Katika mwaka wa nane wa utawala wa mfalme wa Babeli, akamchukua Yehoyakini kuwa mfungwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maofisa wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na Yehoyakini mfalme wa Yuda alijisalimisha kwa mfalme wa Babuloni, yeye mwenyewe pamoja na mama yake, watumishi wake, maofisa na maakida wake. Mfalme wa Babuloni alimchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Yoyakini, mfalme wa Wayuda, alipomtokea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake na watumishi wake na wakuu wake na watumishi wake wa nyumbani, naye mfalme wa Babeli akamchukua katika mwaka wa 8 wa ufalme wake yeye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na Yoyakini mufalme wa Yuda alijitoa kwa mufalme wa Babeli, yeye mwenyewe pamoja na mama yake, watumishi wake, wakubwa na majemadari wake. Mufalme wa Babeli aliwapeleka kama wafungwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.