2 Kings 24:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile, pia kama Mwenyezi-Mungu alivyosema, Nebukadneza alichukua mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na ndani ya ikulu. Alikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alitengeneza. Vyombo hivyo vilikuwa ndani ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akatoa huko hazina zote za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikata-kata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivifanya katika hekalu la Bwana, kama Bwana alivyosema.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile, pia kama Mwenyezi-Mungu alivyosema, Nebukadneza alichukua mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na ndani ya ikulu. Alikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alitengeneza. Vyombo hivyo vilikuwa ndani ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama vile BWANA alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la BWANA na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama vile bwana alivyokuwa amesema, Nebukadneza akaondoa hazina yote kutoka Hekalu la bwana na kutoka jumba la mfalme, akavichukua vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alikuwa amevitengeneza kwa ajili ya Hekalu la bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akatoa huko hazina zote za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama BWANA alivyosema.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile, pia kama Mwenyezi-Mungu alivyosema, Nebukadneza alichukua mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu, na ndani ya ikulu. Alikatakata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Solomoni mfalme wa Israeli alitengeneza. Vyombo hivyo vilikuwa ndani ya hekalu la Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatoa navyo vilimbiko vyote vya Nyumba ya Bwana na vilimbiko vya nyumba ya mfalme, dhahabu na vyombo vyote, Salomo, mfalme wa Waisiraeli, alivyovitengeneza vya kutumiwa Jumbani mwa Bwana, akavivunjavunja, kama Bwana alivyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akatoa huko hazina zote za nyumba ya BWANA, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikata-kata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivifanya katika hekalu la BWANA, kama BWANA alivyosema.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena kama vile Yawe alivyosema, Nebukadneza alitwaa mali yote iliyokuwa ndani ya nyumba ya Yawe, na ndani ya nyumba ya kifalme. Akakatakata vyombo vyote vya zahabu ambavyo Solomono mufalme wa Israeli alitengeneza. Vyombo hivyo vilikuwa ndani ya hekalu la Yawe.