2 Kings 24:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimchukua Yehoyakini mpaka Babuloni pamoja na mama yake mfalme, wake za mfalme, maofisa wake na wakuu wa nchi; wote hao aliwatoa Yerusalemu, akawapeleka Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimchukua Yehoyakini mpaka Babuloni pamoja na mama yake mfalme, wake za mfalme, maofisa wake na wakuu wa nchi; wote hao aliwatoa Yerusalemu, akawapeleka Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini kwenda Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu kwenda Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake na viongozi wote wa nchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nebukadneza akamchukua mateka Yehoyakini hadi Babeli. Pia akawachukua utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli mama yake mfalme, wake zake, maafisa wake, na viongozi wote wa nchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maofisa wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alimchukua Yehoyakini mpaka Babuloni pamoja na mama yake mfalme, wake za mfalme, maofisa wake na wakuu wa nchi; wote hao aliwatoa Yerusalemu, akawapeleka Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Yoyakini akamhamisha kwenda Babeli na mamake mfalme na wakeze mfalme na watumishi wake wa nyumbani, nao wenye macheo katika nchi hii akawatoa Yerusalemu na kuwapeleka Babeli kifungoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alimupeleka Yoyakini mpaka Babeli pamoja na mama ya mufalme, wake za mufalme, wakubwa wa waaskari wake, na wakubwa wa inchi wote. Hao aliwatoa Yerusalema. Akawapeleka katika uhamisho kule Babeli.