2 Kings 24:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu akampelekea makundi ya Wababuloni, Waaramu, Wamoabu na Waamoni washambulie nchi ya Yuda na kuiharibu, kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu alilolisema kwa watumishi wake manabii.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na watumishi wake manabii.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu akampelekea makundi ya Wababuloni, Waaramu, Wamoabu na Waamoni washambulie nchi ya Yuda na kuiharibu, kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu alilolisema kwa watumishi wake manabii.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA akatuma Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia ghafula. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la BWANA lililosemwa na watumishi wake manabii.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana akatuma wavamiaji wa Wakaldayo, Waaramu, Wamoabu na Waamoni ili kumshambulia. Aliwatuma kuiangamiza Yuda sawasawa na neno la bwana lililosemwa na watumishi wake manabii.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu akampelekea makundi ya Wababuloni, Waaramu, Wamoabu na Waamoni washambulie nchi ya Yuda na kuiharibu, kulingana na neno la Mwenyezi-Mungu alilolisema kwa watumishi wake manabii.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana alipotuma kwake vikosi vya Wakasidi na vikosi vya Washami na vikosi vya Wamoabu na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma katika nchi ya Yuda, waiangamize kwa lile neno la Bwana, alilolisema vinywani mwa watumishi wake wafumbuaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akamupelekea makundi ya Wababeli, Waaramu, Wamoabu na Waamoni washambulie inchi ya Yuda na kuiharibu, kulingana na neno la Yawe alilolisema kwa njia ya watumishi wake manabii.