2 Kings 24:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu aliwakasirikia sana watu wa Yerusalemu na Yuda, hata akawafukuza mbali naye. Sedekia alimwasi mfalme wa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haya yote yalitendeka Yerusalemu na Yuda kwa sababu ya hasira ya Mwenyezi Mungu, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana kwa sababu ya hasira ya Bwana mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu aliwakasirikia sana watu wa Yerusalemu na Yuda, hata akawafukuza mbali naye. Sedekia alimwasi mfalme wa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya BWANA haya yote yakatokea katika Yerusalemu na katika Yuda, na mwishoni akawasukumia mbali na uso wake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ilikuwa ni kwa sababu ya hasira ya bwana haya yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, naye mwishoni akawaondoa mbele zake. Basi, Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana kwa sababu ya hasira ya BWANA mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu aliwakasirikia sana watu wa Yerusalemu na Yuda, hata akawafukuza mbali naye. Sedekia alimwasi mfalme wa Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ikawa kwa ajili ya makali ya Bwana yaliyouwakia mji wa Yerusalemu, hata nchi ya Yuda, akiwatupa, waondoke usoni pake. Kisha Sedekia akamkataa mfalme wa Babeli akiacha kumtii.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana kwa sababu ya hasira ya BWANA mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe aliwakasirikia sana watu wa Yerusalema na Yuda, hata akawafukuza mbali naye. Zedekia alimwasi mufalme wa Babeli.