2 Kings 25:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi wa mwaka wa tisa wa utawala wake Sedekia, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake, akaushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira na kujenga ngome kuuzunguka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli, akiwa na jeshi lake lote, alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzingira pande zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa katika mwaka wa kenda wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi wa mwaka wa tisa wa utawala wake Sedekia, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake, akaushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira na kujenga ngome kuuzunguka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli akaenda kupigana dhidi ya Yerusalemu pamoja na jeshi lake lote. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzunguka kwa jeshi kote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo katika mwaka wa tisa wa utawala wa Sedekia, katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, Nebukadneza mfalme wa Babeli, akiwa na jeshi lake lote, alifanya vita dhidi ya Yerusalemu. Akapiga kambi nje ya mji na kuuzunguka mji pande zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa katika mwaka wa tisa wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi wa mwaka wa tisa wa utawala wake Sedekia, Nebukadneza mfalme wa Babuloni alifika na jeshi lake, akaushambulia mji wa Yerusalemu, akauzingira na kujenga ngome kuuzunguka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwaka wa 9 wa ufalme wake katika mwezi wa kumi siku ya kumi ya mwezi, ndipo, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, alipoujia Yerusalemu yeye na vikosi vyake vyote, wakapiga makambi huko, wakaujengea boma la kuuzungusha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa katika mwaka wa kenda wa kutawala kwake, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaja, yeye na jeshi lake lote, kupigana na Yerusalemu, akapanga hema zake kuukabili; nao wakajenga ngome juu yake pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya kumi ya mwezi wa kumi, mwaka wa tisa wa utawala wa Zedekia, Nebukadneza mufalme wa Babeli akafika na waaskari wake kwa kushambulia Yerusalema. Akapiga kambi mbele ya muji ule na kujenga ngazi kuuzunguka.