2 Kings 25:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebakia mjini na wale wote waliokuwa wamejisalimisha kwa mfalme wa Babuloni pamoja na watu wengine wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebakia mjini na wale wote waliokuwa wamejisalimisha kwa mfalme wa Babuloni pamoja na watu wengine wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nebuzaradani jemadari wa jeshi la walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na watu wengine waliokuwa wamebaki, na wale askari waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi akawapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebaki katika mji, pamoja na mabaki ya watu wa kawaida, na wale waliojisalimisha kwa mfalme wa Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, akawachukua mateka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliwapeleka uhamishoni watu waliokuwa wamebakia mjini na wale wote waliokuwa wamejisalimisha kwa mfalme wa Babuloni pamoja na watu wengine wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Masao ya watu waliosalia mjini nao waliokuwa wamemwangukia mfalme wa Babeli na kurudi upande wake, hayo masao yote ya mtutumo wa watu Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, akawateka na kuwahamisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mabaki ya watu waliosalia katika mji, nao wale walioasi, na kumkimbilia mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu wote wengine, watu hao Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, akawachukua mateka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nebuzaradani, mukubwa wa waaskari wa mufalme, akawapeleka katika uhamisho watu waliokuwa wamebakia katika muji na wale wote waliokuwa wamejitoa wenyewe kwa mufalme wa Babeli pamoja na watu wengine wote.