2 Kings 25:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, pamoja na vikalio vyake, birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi mpaka Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakaldayo walivunja vipande vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Hivyo wakaichukua hiyo shaba na kuipeleka Babeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa Bwana, na matako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa Bwana, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, pamoja na vikalio vyake, birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi mpaka Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakaldayo wakavunja zile nguzo za shaba, vishikilio vya shaba vinavyohamishika na ile Bahari ya shaba, vile vitu ambavyo vilikuwa katika Hekalu la BWANA, nao wakaichukua hiyo shaba kwenda Babeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakaldayo walivunja vipande zile nguzo za shaba, vile vishikilio vya shaba vilivyohamishika, na ile Bahari ya shaba, ambavyo vyote vilikuwa katika Hekalu la bwana. Hivyo wakaichukua hiyo shaba na kuipeleka Babeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na vitako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakaldayo walivunja vipandevipande nguzo za shaba ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, pamoja na vikalio vyake, birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwamo katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, wakaichukua shaba nyeusi mpaka Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini zile nguzo mbili za shaba zilizokuwa penye Nyumba ya Bwana na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji na bahari ya shaba iliyokuwa penye Nyumba ya Bwana Wakasidi wakazivunja, nazo zile shaba zao wakazipeleka Babeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na zile nguzo za shaba zilizokuwako nyumbani mwa BWANA, na matako, na ile bahari ya shaba, iliyokuwamo nyumbani mwa BWANA, Wakaldayo wakavivunja vipande vipande, wakaichukua shaba yake yote mpaka Babeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wababeli walivunja vipandevipande nguzo za shaba ambazo zilikuwa katika nyumba ya Yawe, pamoja na viikalio vya birika kubwa la shaba nyeusi lililokuwa mule katika nyumba ya Yawe, wakapeleka shaba nyeusi mpaka Babeli.