2 Kings 25:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, ilikuwa na uzito mwingi usioweza kupimika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na yale matako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya Bwana; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Solomoni alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la BWANA, ilikuwa nzito kiasi kwamba haikuweza kupimika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shaba iliyotokana na zile nguzo mbili, ile Bahari na vile vishikilio vilivyohamishika, ambavyo Sulemani alikuwa ametengeneza kwa ajili ya Hekalu la bwana, ilikuwa na uzito usioweza kupimika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na vile vitako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Shaba yote nyeusi aliyotumia Solomoni kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na vikalio kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu haikuweza kupimwa kwa uzito.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Zile nguzo mbili na ile bahari moja na vile vilingo vya kuwekea mitungi ya maji, ambavyo mfalme Salomo alivitengenezea Nyumba ya Bwana, shaba zao hivi vyombo vyote hazikuwezekana kupimwa kwa mizani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Zile nguzo mbili, na ile bahari moja, na yale matako, Sulemani alivyoifanyia nyumba ya BWANA; shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Shaba yote nyeusi Solomono aliyotumia kwa kutengeneza zile nguzo mbili, birika lile kubwa na viikalio kwa ajili ya nyumba ya Yawe haikuweza kupimwa kwa uzito.