2 Kings 25:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
alimchukua towashi mmoja huko mjini ambaye alikuwa akiwaongoza askari vitani, pamoja na watu watano mashuhuri wa mfalme ambao aliwakuta huko. Vilevile, alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu sitini mashuhuri ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua kiongozi wa wapiganaji, na washauri watano wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na katika mji akamtwaa towashi mmoja, aliyewasimamia watu wa vita; na watu watano katika wale waliosimama mbele ya mfalme, walioonekana mjini; na katibu wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana mjini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
alimchukua towashi mmoja huko mjini ambaye alikuwa akiwaongoza askari vitani, pamoja na watu watano mashuhuri wa mfalme ambao aliwakuta huko. Vilevile, alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu sitini mashuhuri ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miongoni mwa wale ambao bado walikuwa katika mji, akamchukua afisa aliyesimamia mashujaa na washauri watano wa kifalme. Akamchukua pia mwandishi ambaye alikuwa afisa aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliokutwa ndani ya mji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miongoni mwa wale watu waliokuwa wamesalia katika mji, alimchukua afisa kiongozi wa wapiganaji, na washauri watano wa mfalme. Akamchukua pia mwandishi aliyesimamia uandikishaji wa watu wa nchi, pamoja na watu wake sitini waliopatikana ndani ya mji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na katika mji akamtwaa towashi mmoja, aliyewasimamia watu wa vita; na watu watano katika wale waliosimama mbele ya mfalme, walioonekana mjini; na katibu wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana mjini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
alimchukua towashi mmoja huko mjini ambaye alikuwa akiwaongoza askari vitani, pamoja na watu watano mashuhuri wa mfalme ambao aliwakuta huko. Vilevile, alimchukua katibu wa kamanda mkuu wa jeshi ambaye alitunza kumbukumbu za jeshi pamoja na watu sitini mashuhuri ambao aliwakuta mjini Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo mjini akachukua mtumishi mmoja wa nyumbani mwa mfalme aliyewekwa kuwa mkuu wa kuwasimamia wapiga vita na watu watano waliokuwa na kazi machoni pa mfalme waliopatikana mjini na mwandishi wa mkuu wa vikosi aliyewaandika watu wa nchi waliotakiwa uaskari na watu sitini wa shambani waliopatikana mle mjini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na katika mji akamtwaa towashi mmoja, aliyewasimamia watu wa vita; na watu watano katika wale waliosimama mbele ya mfalme, walioonekana mjini; na katibu wa jemadari wa jeshi, aliyewaandika watu wa nchi; na watu sitini katika watu wa nchi, walioonekana mjini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamupeleka jemadari mumoja kule katika muji ambaye alikuwa akiwaongoza waaskari katika vita, pamoja na watu watano wenye heshima wa mufalme ambao aliwakuta kule. Vilevile, akamupeleka katibu wa jemadari wa waaskari ambaye alichunga habari za kuandika waaskari wapya pamoja na watu makumi sita wenye heshima ambao aliwakuta Yerusalema.