2 Kings 25:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, kuwa mtawala wa watu wote wa Yuda ambao hawakupelekwa Babuloni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa habari ya watu waliosalia katika nchi ya Yuda, aliowasaza Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani awe liwali juu yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, kuwa mtawala wa watu wote wa Yuda ambao hawakupelekwa Babuloni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nebukadneza mfalme wa Babeli akamteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, awe msimamizi wa watu aliowaacha Yuda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kwa habari ya watu waliosalia katika nchi ya Yuda, aliowasaza Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani awe mtawala juu yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Nebukadneza wa Babuloni alimteua Gedalia mwana wa Ahikamu, mjukuu wa Shafani, kuwa mtawala wa watu wote wa Yuda ambao hawakupelekwa Babuloni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wale watu waliosalia katika nchi ya Yuda, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliowasaza, akawawekea Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, kuwasimamia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa habari ya watu waliosalia katika nchi ya Yuda, aliowasaza Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani awe liwali juu yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Nebukadneza wa Babeli akamuchagua Gedalia mwana wa Ahikamu, mujukuu wa Safanu, kuwa mutawala wa watu wote wa Yuda ambao hawakupelekwa Babeli.