2 Kings 25:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha makapteni wote wa majeshi pamoja na watu wao waliposikia kuwa mfalme wa Babuloni alimteua Gedalia kuwa mtawala, walimwendea Gedalia huko Mizpa. Watu hao walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kuwa mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa liwali, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha makapteni wote wa majeshi pamoja na watu wao waliposikia kuwa mfalme wa Babuloni alimteua Gedalia kuwa mtawala, walimwendea Gedalia huko Mizpa. Watu hao walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kama mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa, nao ni Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia kuwa mtawala, wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa mtawala, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha makapteni wote wa majeshi pamoja na watu wao waliposikia kuwa mfalme wa Babuloni alimteua Gedalia kuwa mtawala, walimwendea Gedalia huko Mizpa. Watu hao walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wote wa vikosi, wao na watu wao, waliposikia, ya kuwa mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwasimamia, wakaja Misipa kwa Gedalia; ndio Isimaeli, mwana wa Netania, na Yohana, mwana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanumeti, wa Netofa, na Yazania, mwana wa mtu wa Maka, hao wenyewe na watu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kisha, wakuu wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemweka Gedalia kuwa liwali, wakamwendea Gedalia huko Mispa; nao ni hawa, Ishmaeli mwana wa Nethania, na Yohana mwana wa Karea, na Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka, wao na watu wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha wakubwa wote wa waaskari pamoja na watu wao waliposikia kwamba mufalme wa Babeli alimuchagua Gedalia kuwa mutawala, wakamwendea Gedalia kule Mispa. Watu hao walikuwa ni: Isimaeli mwana wa Netania, Yohana mwana wa Karea, Seraya mwana wa Taumeti wa muji wa Netofati, na Yazania mwana wa Mumakati.