2 Kings 25:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, sehemu ya ukuta wa mji ilibomolewa, nao askari wote wakakimbia wakati wa usiku wakipitia katika bustani ya mfalme kwenye lango katikati ya kuta mbili, wakaenda upande wa Araba, ingawa Wababuloni walikuwa wameuzunguka mji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, sehemu ya ukuta wa mji ilibomolewa, nao askari wote wakakimbia wakati wa usiku wakipitia katika bustani ya mfalme kwenye lango katikati ya kuta mbili, wakaenda upande wa Araba, ingawa Wababuloni walikuwa wameuzunguka mji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, jeshi lote likakimbia usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha ukuta wa mji ukavunjwa, na jeshi lote likakimbia. Wakaondoka mjini usiku kupitia lango lililokuwa kati ya kuta mbili karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Wakakimbia kuelekea Araba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, sehemu ya ukuta wa mji ilibomolewa, nao askari wote wakakimbia wakati wa usiku wakipitia katika bustani ya mfalme kwenye lango katikati ya kuta mbili, wakaenda upande wa Araba, ingawa Wababuloni walikuwa wameuzunguka mji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mji ulipobomolewa, nao wapiga vita wote wakatoroka usiku huo kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili penye bustani ya mfalme, nao Wakasidi walikuwa wamelala na kuuzunguka mji, wale wakishika njia ya nyikani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, sehemu ya ukuta wa muji ukabomolewa, naye mufalme pamoja na waaskari wote wakakimbia wakati wa usiku wakipitia katika bustani ya mufalme kwenye mulango katikati ya kuta mbili, wakaenda upande wa Araba, ingawa Wababeli walikuwa wameuzunguka muji.