2 Kings 25:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika siku ya saba ya mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliingia Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ya saba ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani mkuu wa askari walinzi wa mfalme, afisa wa mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika siku ya saba ya mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliingia Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya saba ya mwezi wa tano katika mwaka wa kumi na tisa wa kutawala kwake Mfalme Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani jemadari wa jeshi la walinzi wa mfalme na afisa wa mfalme wa Babeli, wakaja Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnamo siku ya saba ya mwezi wa tano, katika mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani jemadari wa askari walinzi wa mfalme, afisa wa mfalme wa Babeli, alikuja Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na tisa wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, kamanda wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika siku ya saba ya mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babuloni, Nebuzaradani kapteni wa walinzi wa mfalme, aliingia Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwezi wa tano siku ya saba ya mwezi-ulikuwa mwaka wa 19 wa mfalme Nebukadinesari, mfalme wa Babeli-ndipo, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, mtumishi wa mfalme wa Babeli, alipoingia Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata mwezi wa tano, siku ya saba ya mwezi, ndio mwaka wa kumi na kenda wa mfalme Nebukadreza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, amiri wa askari walinzi, mtumishi wa mfalme wa Babeli, akaingia Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya saba ya mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadneza mufalme wa Babeli, Nebuzaradani mukubwa wa waaskari walinzi wa mufalme, akaingia Yerusalema.