2 Kings 3:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa mfalme Yehoshafati wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala Israeli, akatawala kutoka Samaria kwa muda wa miaka kumi na miwili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoramu mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na mbili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi Yoramu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa mfalme Yehoshafati wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala Israeli, akatawala kutoka Samaria kwa muda wa miaka kumi na miwili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoramu mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa kutawala kwake Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoramu mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli katika Samaria mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa mfalme Yehoshafati wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala Israeli, akatawala kutoka Samaria kwa muda wa miaka kumi na miwili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yoramu, mwana wa Ahabu, akapata kuwa mfalme wa Waisiraeli huko Samaria katika mwaka wa 18 wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, akawa mfalme miaka 12.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka kumi na miwili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa mufalme Yosafati wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala inchi ya Israeli. Akatawala akiwa Samaria kwa muda wa miaka kumi na miwili.