2 Kings 3:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elisha akamwuliza mfalme wa Israeli, “Nina uhusiano gani nawe? Nenda ukawatake shauri manabii ambao baba yako na mama yako waliwaendea.” Mfalme wa Israeli akajibu, “Sivyo! Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetuita sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa mfalme wa Moabu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Al-Yasa akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina uhusiano gani nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” Mfalme wa Israeli akajibu, “La, sivyo, kwa sababu ni Mwenyezi Mungu ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa Bwana amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elisha akamwuliza mfalme wa Israeli, “Nina uhusiano gani nawe? Nenda ukawatake shauri manabii ambao baba yako na mama yako waliwaendea.” Mfalme wa Israeli akajibu, “Sivyo! Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetuita sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa mfalme wa Moabu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina nini mimi nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” Mfalme wa Israeli akajibu, “La hasha, kwa sababu ni BWANA ambaye ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Al-Yasa akamwambia mfalme wa Israeli, “Nina nini mimi nawe? Nenda kwa manabii wa baba yako na manabii wa mama yako.” Mfalme wa Israeli akajibu, “La hasha, kwa sababu ni bwana ambaye ametuita pamoja sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa Moabu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elisha akamwuliza mfalme wa Israeli, “Nina uhusiano gani nawe? Nenda ukawatake shauri manabii ambao baba yako na mama yako waliwaendea.” Mfalme wa Israeli akajibu, “Sivyo! Mwenyezi-Mungu ndiye aliyetuita sisi wafalme watatu ili atutie mikononi mwa mfalme wa Moabu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elisa akamwambia mfalme wa Waisiraeli: Tuna bia gani mimi na wewe? Nenda kwa wafumbuaji wa baba yako na kwa wafumbuaji wa mama yako! Mfalme wa Waisiraeli akamwambia: La! Kweli Bwana amewaita hawa wafalme, awatie mikononi mwa Wamoabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elisha akamwuliza mufalme wa Israeli: “Kuna maneno gani kati yako nami? Kwenda uombe shauri kwa manabii ambao baba yako na mama yako waliwaendea.” Mufalme wa Israeli akajibu: “Sivyo! Yawe ndiye aliyetuita sisi wafalme watatu kusudi atutie katika mikono ya mufalme wa Moabu.”