2 Kings 3:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elisha akasema, “Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu ambaye mimi ninamtumikia, naapa kwamba kama isingekuwa kwa heshima niliyo nayo kwa rafiki yako mfalme Yehoshafati wa Yuda, nisingekujali hata kidogo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Al-Yasa akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni aishivyo, ninayemtumikia, kama si kwa heshima niliyo nayo kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekujali hata kidogo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elisha akasema, “Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu ambaye mimi ninamtumikia, naapa kwamba kama isingekuwa kwa heshima niliyo nayo kwa rafiki yako mfalme Yehoshafati wa Yuda, nisingekujali hata kidogo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Elisha akasema, “Hakika, kama BWANA Mwenye Nguvu Zote aishivyo, ambaye ninamtumikia, kama si kuheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekutazama wala hata kukutupia jicho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Al-Yasa akasema, “Hakika, kama bwana Mwenye Nguvu Zote aishivyo ambaye ninamtumikia, kama si kuheshimu Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekutazama wala hata kukutupia jicho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Elisha akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama nisingemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingekutazama, wala kuonana nawe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elisha akasema, “Kama aishivyo Mwenyezi-Mungu mwenye nguvu ambaye mimi ninamtumikia, naapa kwamba kama isingekuwa kwa heshima niliyo nayo kwa rafiki yako mfalme Yehoshafati wa Yuda, nisingekujali hata kidogo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Elisa akasema: Hivyo, Bwana Mwenye vikosi alivyo Mwenye uzima, ambaye ninasimama mbele yake, kama nisingeutazama uso wa Yosafati, mfalme wa Wayuda, wewe nisingekuelekezea macho, nisikuone!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Elisha akasema, Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elisha akasema: “Kama vile Yawe wa majeshi, yule ambaye mimi ninamutumikia, anavyoishi, kama isingekuwa kwa heshima ninayokuwa nayo kwa rafiki yako mufalme Yosafati wa Yuda, nisingekujali hata kidogo.