2 Kings 4:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu amefariki, na kama ujuavyo, alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia fedha amekuja kuwatwaa wanangu wawili wawe watumwa wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Al-Yasa, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha Mwenyezi Mungu. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu amefariki, na kama ujuavyo, alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia fedha amekuja kuwatwaa wanangu wawili wawe watumwa wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mke wa mtu mmoja kutoka katika wana wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako mume wangu amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha BWANA. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Al-Yasa, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha bwana. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemdai amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu amefariki, na kama ujuavyo, alikuwa mcha Mungu, lakini aliyemwia fedha amekuja kuwatwaa wanangu wawili wawe watumwa wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kulikuwa na mwanamke wa wanafunzi wa wafumbuaji, akamlilia Elisa kwamba: Mume wangu, mtumishi wako, amekufa, nawe unajua, ya kuwa mtumishi wako alikuwa mwenye kumcha Bwana; tena mtu, aliyemkopa, amekuja kuwachukua wanangu mawili, wawe watumwa wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mwanamuke mumoja kati ya wake za wanafunzi wa manabii akamwendea Elisha, akamwambia: “Mutumishi wako, mume wangu amekufa, na kama vile unavyojua, alikuwa mwenye kumwogopa Mungu. Lakini mutu aliyemukopesha feza amekuja kuwatwaa wana wangu wawili wakuwe watumwa wake.”