2 Kings 4:27 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipofika mlimani kwa mtu wa Mungu akamshika miguu, naye Gehazi akakaribia ili amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, “Mwache, kwani ana uchungu mkali, naye Mwenyezi-Mungu hakunijulisha jambo hilo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipomfikia huyo mtu wa Mungu pale mlimani, akashika miguu yake. Gehazi akaja ili amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akasema, “Mwache! Yuko katika uchungu mkubwa, lakini Mwenyezi Mungu amenificha jambo hili na hajaniambia kwa nini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na Bwana amenificha, wala hakuniambia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipofika mlimani kwa mtu wa Mungu akamshika miguu, naye Gehazi akakaribia ili amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, “Mwache, kwani ana uchungu mkali, naye Mwenyezi-Mungu hakunijulisha jambo hilo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipomfikia huyo mtu wa Mungu pale mlimani, akashika miguu yake. Gehazi akaja ili amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akasema, “Mwache! Yuko katika uchungu mkubwa, lakini BWANA amenificha jambo hili na hajaniambia kwa nini.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipomfikia huyo mtu wa Mungu pale mlimani, akashika miguu yake. Gehazi akaja ili amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akasema, “Mwache! Yuko katika uchungu mkubwa, lakini bwana amenificha jambo hili na hajaniambia kwa nini.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipofika mlimani kwa mtu wa Mungu akamshika miguu, naye Gehazi akakaribia ili amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, “Mwache, kwani ana uchungu mkali, naye Mwenyezi-Mungu hakunijulisha jambo hilo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipofika mlimani kwake yule mtu wa Mungu akamshika miguu; ndipo, Gehazi alipokuja, amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akamwambia: Mwache! Kwani anayo machungu rohoni; naye Bwana amenificha jambo hili, hakuniambia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipofika kwenye mulima kwa mutu wa Mungu, akamushika miguu, naye Gehazi akakaribia kusudi amwondoe. Lakini mutu wa Mungu akamwambia: “Umwache, maana ana uchungu mukali, naye Yawe hakunijulisha jambo hilo.”