2 Kings 4:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Elisha akamwambia Gehazi, “Chukua fimbo yangu, uondoke mara moja. Usisimame njiani kumwamkia mtu yeyote, na mtu yeyote akikuamkia njiani, usipoteze wakati kurudisha salamu. Nenda moja kwa moja mpaka nyumbani na kuweka fimbo yangu juu ya mtoto.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Al-Yasa akamwambia Gehazi, “Jikaze viuno, chukua fimbo yangu mkononi mwako na ukimbie. Ikiwa utakutana na mtu yeyote, usimsalimie, na mtu yeyote akikusalimu, usimjibu. Ilaze fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Elisha akamwambia Gehazi, “Chukua fimbo yangu, uondoke mara moja. Usisimame njiani kumwamkia mtu yeyote, na mtu yeyote akikuamkia njiani, usipoteze wakati kurudisha salamu. Nenda moja kwa moja mpaka nyumbani na kuweka fimbo yangu juu ya mtoto.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Elisha akamwambia Gehazi, “Jikaze viuno, chukua fimbo yangu mkononi mwako na ukimbie. Ikiwa utakutana na mtu ye yote, usimsalimie, na mtu ye yote akikusalimu, usimjibu. Ilaze fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Al-Yasa akamwambia Gehazi, “Jikaze viuno, chukua fimbo yangu mkononi mwako na ukimbie. Ikiwa utakutana na mtu yeyote, usimsalimie, na mtu yeyote akikusalimu, usimjibu. Ilaze fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Elisha akamwambia Gehazi, “Chukua fimbo yangu, uondoke mara moja. Usisimame njiani kumwamkia mtu yeyote, na mtu yeyote akikuamkia njiani, usipoteze wakati kurudisha salamu. Nenda moja kwa moja mpaka nyumbani na kuweka fimbo yangu juu ya mtoto.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Elisa akamwambia Gehazi: Funga viuno vyako, uichukue fimbo yangu mkononi mwako, uende! Ukiona mtu, usimwamkie! Kama anakuamkia, usimjibu! Uiweke fimbo yangu usoni pa mtoto!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, Jikaze viuno, ukachukue fimbo yangu mkononi mwako, ukaende zako; ukikutana na mtu, usimsalimu; na mtu akikusalimu, usimjibu; ukaweke fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Elisha akamwambia Gehazi: “Ujitayarishe kusafiri, twaa fimbo yangu, na uende mara moja. Usisimame katika njia kwa kumusalimia mutu yeyote, na mutu yeyote akikusalimia katika njia, usipoteze wakati kwa kumurudishia salamu. Kwenda moja kwa moja mpaka katika nyumba na kuweka fimbo yangu juu ya uso wa mutoto.”