2 Kings 4:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwanamke akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe uishivyo, sitakuacha.” Basi Elisha akaondoka na kufuatana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini mama mtoto akasema, “Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo Al-Yasa akainuka, akafuatana naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mama yake yule mtoto akasema, Kama Bwana aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwanamke akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe uishivyo, sitakuacha.” Basi Elisha akaondoka na kufuatana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini mama wa mtoto akasema, “Hakika kama BWANA aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo Elisha akainuka, akafuatana naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini mama mtoto akasema, “Hakika kama bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo Al-Yasa akainuka, akafuatana naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mama yake yule mtoto akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwanamke akamwambia Elisha, “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo na kama wewe uishivyo, sitakuacha.” Basi Elisha akaondoka na kufuatana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mama ya mtoto aliposema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, tena hivyo, wewe mwenyewe ulivyo mzima, sitakuacha kabisa! Ndipo, alipoinuka kufuatana naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mama yake yule mtoto akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Basi akaondoka, akamfuata.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwanamuke akamwambia Elisha: “Kama vile Yawe anavyoishi na kama vile unavyoishi, sitakuacha.” Basi Elisha akaondoka na kufuatana naye.