2 Kings 4:39 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mmoja wao akaenda shambani na kuchuma mboga. Huko akaona mtango-mwitu, akachuma matango mengi kadiri alivyoweza kuchukua. Akaja nayo, akayakatakata na kuyatia chunguni bila kuyajua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mmoja wao akatoka kwenda mashambani kuchuma mboga na akapata mtango-mwitu. Akachuma matango na kujaza nguo yake aliyoikunja ili kubebea. Aliporudi, akayakatakata na kuyatumbukiza ndani ya chungu, ingawa hakuna aliyejua ni nini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mmoja wao akaenda shambani na kuchuma mboga. Huko akaona mtango-mwitu, akachuma matango mengi kadiri alivyoweza kuchukua. Akaja nayo, akayakatakata na kuyatia chunguni bila kuyajua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mmoja wao akatoka kwenda mashambani kuchuma mboga na akapata mtango mwitu. Akachuma matango na kujaza nguo yake aliyoikunja ili kubebea. Aliporudi, akayakatakata na kuyatumbukiza ndani ya chungu, ingawa hakuna aliyejua ni nini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mmoja wao akatoka kwenda mashambani kuchuma mboga na akapata mtango mwitu. Akachuma matango na kujaza nguo yake aliyoikunja ili kubebea. Aliporudi, akayakatakata na kuyatumbukiza ndani ya chungu, ingawa hakuna aliyejua ni nini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtangomwitu, akayachuma matangomwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasuapasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mmoja wao akaenda shambani na kuchuma mboga. Huko akaona mtango-mwitu, akachuma matango mengi kadiri alivyoweza kuchukua. Akaja nayo, akayakatakata na kuyatia chunguni bila kuyajua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mmoja akaenda shambani, akachuma mboga, akaona mtango wa mwituni, akachuma kwake hayo matango ya mwituni, akaijaza nguo yake, kisha akaja, akayakatakata chunguni kuwa chakula, kwani hawakuyajua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtango-mwitu, akayachuma matango-mwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasua-pasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mumoja wao akaenda katika shamba na kuchuma mboga. Kule akaona mboga za pori, akachuma mboga nyingi kwa kadiri alivyoweza kubeba. Akakuja nazo, akazikatakata na kuzitia ndani ya chungu bila kuzijua.