2 Kings 4:42 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtu Mmoja akatoka Baal-shalisha, akamletea Elisha mikate ishirini iliyotengenezwa kwa shayiri ya malimbuko ya mavuno ya mwaka huo na masuke mabichi ya ngano guniani. Elisha akamwagiza Gehazi awape watu wale.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutoka kwa nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Al-Yasa akasema, “Wape watu ili wale.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtu Mmoja akatoka Baal-shalisha, akamletea Elisha mikate ishirini iliyotengenezwa kwa shayiri ya malimbuko ya mavuno ya mwaka huo na masuke mabichi ya ngano guniani. Elisha akamwagiza Gehazi awape watu wale.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Elisha akasema, “Wape watu ili wale.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Al-Yasa akasema, “Wape watu ili wale.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtu Mmoja akatoka Baal-shalisha, akamletea Elisha mikate ishirini iliyotengenezwa kwa shayiri ya malimbuko ya mavuno ya mwaka huo na masuke mabichi ya ngano guniani. Elisha akamwagiza Gehazi awape watu wale.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaja mtu kutoka Baali-Salisa, akamletea yule mtu wa Mungu mikate ya malimbuko, nayo ilikuwa mikate ishirini ya mawele, tena gunia lenye masuke mabichi, akasema: Wapeni, watu hawa wale!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutu mumoja akatoka Bali-Salisa, akamuletea Elisha mikate makumi mbili iliyotengenezwa kwa shayiri ya malimbuko ya mavuno ya mwaka ule na masuke mabichi ya ngano katika gunia. Elisha akamwagiza Gehazi awape watu wakule.