2 Kings 4:43 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtumishi wake akasema, “Sitawapa kwa sababu hakitawatosha watu 100”. Elisha akasema, “Wape wale, kwa sababu Mwenyezi-Mungu amesema kwamba watakula washibe na kingine kitabaki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia moja?” Lakini Al-Yasa akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Watakula na kusaza.’ ”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandikie hiki watu mia? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa Bwana asema hivi, Watakula na kusaza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtumishi wake akasema, “Sitawapa kwa sababu hakitawatosha watu 100”. Elisha akasema, “Wape wale, kwa sababu Mwenyezi-Mungu amesema kwamba watakula washibe na kingine kitabaki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtumishi wake akamwuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?” Lakini Elisha akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo BWANA: ‘Watakula na kusaza.’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?” Lakini Al-Yasa akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo bwana: ‘Watakula na kusaza.’ ”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandalie hiki watu mia moja? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa BWANA asema hivi, Watakula na kusaza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtumishi wake akasema, “Sitawapa kwa sababu hakitawatosha watu 100”. Elisha akasema, “Wape wale, kwa sababu Mwenyezi-Mungu amesema kwamba watakula washibe na kingine kitabaki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtumishi wake akamwambia: watu mia niwaandalie hii mikate namna gani? Akasema: Wape tu watu hawa, wale! Kwani hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watakula, kisha wasaze.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mtumishi wake akasema, Je! Niwaandikie hiki watu mia? Lakini akasema, Uwape watu, ili wale; kwa kuwa BWANA asema hivi, Watakula na kusaza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutumishi wake akasema: “Sitawapa kwa sababu hakitawatosha watu mia moja”. Elisha akasema: “Uwape wakule, kwa sababu Yawe amesema kwamba watakula na kushiba na kingine kitabaki.”