2 Kings 4:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Naye mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Naye mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yule mwanamke akamwendea yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Nenda ukayauze mafuta haya, ulipe deni lako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akarudi kwa mtu wa Mungu na kumweleza habari hizo. Naye mtu wa Mungu akamwambia, “Nenda ukauze hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wanao mtaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, akaenda kumsimulia yule mtu wa Mungu yaliyokuwa, naye akamwambia: Nenda, uyauze hayo mafuta, umlipe yule anayekudai! Yatakayosalia yatumie wewe na wanao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akarudi kwa mutu wa Mungu na kumweleza habari hiyo. Naye mutu wa Mungu akamwambia: “Kwenda uuzishe hayo mafuta na kulipa madeni yako, ndipo wewe na wana wako mutaishi kwa kutumia hayo yatakayobaki.”